Serikali yatafakari kugawa Jimbo la Mbeya Mjini

NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga ameliambia Bunge kuwa serikali inatafakari maombi ya wabunge kugawa majimbo yao ikiwa ni pamoja na Jimbo la Mbeya Mjini anapotoka Spika Dk Tulia Ackson.

Akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalum Sophia Mwakagenda Bungeni leo Machi 3, 2023, Ummy amesema Dk Tulia ni miongoni mwa Wabunge waliowasilisha maombi ya kutaka majimbo yao yagawanywe kutokana na ukubwa na idadi ya wananchi.

“Serikali inatafakari maombi hayo na wakati utakapofika vigezo vitazingatiwa,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

Back to top button