Serikali yataka usimamizi uchunguzi watoto wenye mahitaji maalum
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Angellah Kairuki amewaagiza maofisa Elimu Maalum nchini kuhakikisha wanasimamia zoezi la uchunguzi wa awali wa watoto ili kubaini watoto wenye mahitaji maalum katika jamii.
Kairuki alitoa rai hiyo katika Chuo Cha Ualimu Patandi wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa maofisa elimu watu wazima na maofisa elimu maalum .
Amewataka kuhakikisha wanatumia vituo vya uchunguzi (Education Support Resource Assessment Centre) na kuwaelekeza watoto wenye mahitaji maalum katika shule stahiki ambazo wanapaswa kupelekwa ili wapate afua stahiki
Pia ameeleza shughuli za usimamizi na uendeshaji wa elimu zihusishe kikamilifu masuala ya elimu maalumu na elimu ya watu wazima kwa kuhakikisha wanashirikiana na viongozi katika jamii katika kuratibu shughuli za elimu ya watu wazima na elimu maalum katika shule za msingi na sekondari