Serikali yatangaza mkakati kumaliza fistula

SERIKALI imetangaza azma ya kutekeleza kwa vitendo mpango wa kuondoa tatizo la ugonjwa wa fistula kwa wanawake wakati wa kujifungua.

Waziri wa afya Ummy Mwalimu alitangaza hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Fistula, ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kwamba mpango huo unalenga kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Profesa Pascal Rugajo alisema kuwa moja ya mipango mikakati katika kutekeleza hilo ni uwepo wa vituo vya kutoa huduma za uzazi salama na huduma za kukabiliana na uzazi pingamizi.

Alisema kuwa hadi sasa huduma za uzazi salama zinatolewa kwenye vituo 503 nchini kwenye vituo vya afya na zahanati na kwamba kwa sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa fistula 21,400 kutoka idadi ya wagonjwa 500,000 waliopo duniani hivyo ni wajibu wa serikali na wadau kuhakikisha wagonjwa hao wanafikiwa na kupata matibabu.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Americares, Dk. Nguke Mwakatundu alisema kuwa changamoto ya fistula nchini bado ni kubwa hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau hawana budi kufanya kazi kwa pamoja na kuongeza juhudi kukabiliana na tatizo hilo.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Americares Dk.Nguke Mwakatundu akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Fistula yaliyofanyika kitaifa wilayani Kasulu mkoani Kigoma(Picha zote na Fadhil Abdallah).

 Dk.Mwakatundu alisema kuwa tangu mwaka 2011 shirika hilo lianze kutoa huduma za afya limewezesha kupatiwa matibabu kwa wagonjwa 2000 katika hospitali ya Bugando na kubainisha kuwa kila mwaka wagonjwa 2500 wanatokea nchini na katib yao wanaopata matibabu ni 1500 tu.

Mwakilishi huyo Mkazi wa Americares alisema kuwa ni lazima huduma za uzazi salama ziimarishwe sambamba na kusogezwa karibu kwa huduma za upasuaji kwa waathirika wa ugonjwa wa fistula.

Kwa upande wake Meneja miradi wa Shirika la CCBRT,Yohana Kaswalala  alisema kuwa tangu mwaka 2003 lilipoanzisha hduma zake nchini shrika hilo limetoa huduma kwa wagonjwa 17500 ambao wameshapata matibabu ya ugionjwa huo. 

Meneja Miradi wa Shirika la CCBRT Yohana Kaswalala akizungumza katika maadhimisho ya Fistula wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi kwenye maadhimisho hayo, Kaswalala alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kuna wanawake zaidi ya 500,000 kusini mwa Jangwa la Sahara ambao wana matatizo ya fistula kati yao 10,000 wakiwa nchini Tanzania hivyo kazi kubwa inatakiwa kufanywa ili kukabiliana na hali hiyo kuweza kurudisha tabasamu kwa wanawake hao.

Alisema kuwa shirika hilo limeendelea kutoa matibabu bure na gharama za usafiri kutoka popote Tanzania kwenda katika hospitali yao jijini Dar es Salaam hivyo kutoa wito kwa wagonjwa wote kujitokeza kupata matibabu.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x