Serikali yatoa Sh bilioni 15 kununua magari ya makamanda wa polisi

SERIKALI imetoa kiasi cha Sh bilioni 15 kwa ajili ya kununua magari ya makamanda wa polisi katika mikoa pamoja na wiliaya (OCD) ili kurahisisha utendaji kazi wa jeshi la polisi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kiasi hicho pia kitahusisha gharama za mafuta kwa magari hayo.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya Polisi, Masauni amewataka askari wahitimu kuwaheshimu Watanzania ikiwa ni pamoja na kutenda haki sambamba na kuyashughulikia matukio ya uhalifu kwa wakati na kwa haraka.

Advertisement