Serikali yawataka maoni mafuta, gesi

SERIKALI imewataka wadau mbalimbali kushiriki katika kutoa maoni juu ya upatikanaji wa mrejesho wa CSR kwenye eneo la mafuta na gesi asilia.

Hayo yamesemwa wakati wa kikao cha wadau kuhusu kupokea maoni juu ya miongozo ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Kikao hicho kimefanyika leo Februari 29, 2024 mkoani Mtwara na kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka mikoa wa Lindi, Mtwara na Pwani.

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema mwanzo utoaji wa CSR ulikuwa ni utashi lakini hauna sheria.

Amesema kwa hao waliyokuwa  wanatoa walitoa kwa matakwa yao bila kuzingatia mahitaji halisi ya maeneo husika hivyo kupitia kikao hicho, maoni yatakayo kusanywa yanaenda kutatua changamoto hizo zilizopo.

“Kwa sisi mtwara ambako gesi inatoka fumefarijika kwamba kikao hiki sasa kinaenda kutoa suluhisho  la namna ya upatikanaji mzuri wa CSR kwa watu wetu na nimefarijika kikao hiki kufanyika ndani ya mkoa wa mtwara, kwetu sisi ni fursa”amesema Abbas

“Naamini baada ya maoni kukusanywa na kufanyiwa kazi sasa tunaenda kupata sheria iliyokuwa mzuri itakayo elekeza namna ya utoaji wa CSR ikiwa ni pamoja na kushirikisha walengwa kwenye maeneo yao”

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petrol (PURA)Charles  Nyangi amesema kikao hicho kina lengo la kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali hasa maeneo ambayo uzalishaji wa gesi asilia yanaendelea na yenye miundombinu.

Aidha viongozi wa maeneo hayo watatakiwa kuandaa miongozo ya uwajibikaji wa makampuni kwenye shughuli za kijamii kwasababu awali ilikuwa kazi hizo zilikuwa zikifanyika bila kuwepo utaratibu maalum.

Mwenyekiti wa Halmshauri ya Mtwara Vijijini, Selemani Nampanye amesema changamoto zilizopo hapo mwanzo ni wananchi kutoshirikishwa katika utekelezaji wa miradi hivyo kupitia kikao hicho uwazi kwa wananchi utapatikana.

Habari Zifananazo

Back to top button