Serikali yaweka mkakati kutatua mgogoro wa miaka 20

GEITA: SERIKALI kupitia Wizara ya Madini imeweka mkakati wa kuhakikisha inatatua mgogoro wa muda mrefu uliodumu zaidi ya miaka 20 tangu kuanza kwa shughuli za uchimbaji madini kati ya wananchi na mgodi unaomilikiwa na Kampuni ya Geita Gold Mine (GGM).

Akizungumza Waziri wa Madini Anthony Mavunde mkoani Geita alipofanya ziara ya kikazi kutembelea maeneo yenye mgogoro wa vigingi na mipasuko baina ya wananchi na mgodi wa GGM amesema mgogoro huo umedumu kwa muda mrefu kitu ambacho sio kizuri.

“Kipekee kabisa, naomba nimshukuru kwa dhati mtangulizi wangu ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dk. Doto Biteko kwa kazi nzuri ambayo alishaianza katika jambo hili.
.
“Kupitia kazi yake, imenifanya mimi kupata mahali pa kuanzia na kazi yangu kuwa nyepesi kuelekea kupata ufumbuzi wa mgogoro huu.” Amesema Mavunde.

Katika maeneo yote ya Nyakabale, Nyamilembo, Samina na Katoma alikotembelea, Mavunde alibainisha kwamba amepata fursa ya kuona hali halisi ya mgogoro huo, na kuahidi kutufanyia kazi na kufika mwisho.

Aidha, Mavunde amesema maoni ya Kamati ya Wataalam, Kamati ya wananchi na GGM alikwisha yaona, aliona ni jambo jema yeye mwenyewe kufika kujionea hali halisi kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button