Serikali yazungumzia kituo cha afya Shitage

SERIKALI imesema inatambua umuhimu wa kuwa na kituo cha afya katika Kata ya Shitage wilayani Uyui, ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 imetenga Sh Milioni 350 kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya Mabama, Loya, Tuura pamoja na Zahanati za Ibela, Mbiti, Izugawima, Gilimba na Magir.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi), Dk Festo Dugange, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Kaskazini, Athuman Almas Maige aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kukamilisha kituo cha afya cha kata hiyo.

Dk Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2025/26 Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Uyui itatenga bajeti kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo cha afya Shitage.

Habari Zifananazo

Back to top button