SGR DAR -Moro wafikia 98.14%

WAZIRI wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema serikali imeendelea na ujenzi wa njia ya Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa ambapo kwa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300) utekelezaji umefikia asilimia 98.

14 na kipande cha Morogoro – Makutupora (km 422) kimefikia asilimia 93.83.

Akisoma Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2023/2024 na Hali ya Uchumi wa Taifa wa mwaka 202215, 2023 Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia Aprili 2023 ujenzi katika kipande cha Makutupora – Tabora (km 371) umefikia asilimia 7.

0, ujenzi wa kipande cha Tabora – Isaka (km 165) umefikia asilimia 2.39; na ujenzi wa kipande cha Mwanza – Isaka (km 341) umefikia asilimia 31.07.

Aidha, amesema mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kukamilika kwa ununuzi wa mabehewa 22 ya abiria kwa ajili ya reli ya kati; kukamilika kwa ukarabati wa mabehewa 52 ya mizigo na mabehewa sita ya abiria na kuanza kutoa huduma katika reli ya kati; na kukamilika kwa uboreshaji wa mfumo wa mawasiliano na umeme katika njia ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Habari Zifananazo

Back to top button