Sh 100 kuongezwa kwa kila lita ya Dizeli, Petroli

SERIKALI imependekeza kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Ushuru wa Barabara na Mafuta, Sura 220 kwa kuongeza Ushuru wa Barabara na Mafuta kwa kiasi cha shilingi 100 kwa kila lita ya mafuta ya Petroli na Dizeli.

Hayo yamesemwa  leo Juni 15, 2023 Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti ya serikali ya mwaka 2023/2024

Amesema, pia anapendekeza kufanya marekebisho kwenye kifungu cha 4A cha Sheria ya Ushuru wa Barabara Sura, 220 kwa kuongeza kipengele ‘c’ kitakachoelekeza fedha zitakazokusanywa kutokana na ongezeko hilo la ushuru wa barabara na mafuta la shilingi 100 kwa mafuta ya petroli na dizeli.

Amesema fedha hizo zitakazokatwa zitatumika kwenye utekelezaji wa miradi ya kimkakati, ili kupata vyanzo vya uhakika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Hatua hii inatarajia kuongeza Mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 381,826.8.”Amesema

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x