Sh 2,350 kwa dakika anakuwa ‘girlfriend’ wako

YOUTUBER wa Marekani mwenye umri wa miaka 23, Caryn Marjorie amejiongezea umaarufu mbali ya kuwa na wafuasi zaidi ya milioni 1.

8 snapchat sasa ana wapenzi zaidi ya 1000 ambao hukaa nao mahali popote kuanzia dakika 10 hadi saa kadhaa kila siku kwa mazungumzo binafsi na yale ya faragha.

Jarida la Fortune limemchapisha, Caryn wiki hii baada ya kuanzisha mtu bandia anayefanana naye CarynAI ambapo watu wanalazimika kulipia Sh 2350 () kwa dakika ili kupiga naye soga.

Kwa wiki moja tangu CarynAI azinduliwe ameingiza kiasi cha dola 71,610 mapato yote yakiwa yanatoka kwa wanaume.

Fortune imeripoti kuwa uandaaji wa tovuti ya CaryAI ulitumia zaidi ya saa 2,000 au siku 83 katika kubuni, kurekodi sauti, tabia na maisha halisi ya Caryn.

“Kwa wanao ingia katika tovuti hiyo, uzoefu unaonesha watu huhisi kuwa wanazungumza moja kwa moja na Caryn,” Fortune imeripoti.

Taarifa zaidi zimesema, CarynAI kwa sasa hawezi kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kila mfuasi wa Caryn hata hivyo utaratibu unafanyika ili kumruhusu kuwasiliana na wafuasi wake walio katika mitandao ya kijamii.

Habari Zifananazo

Back to top button