Sh Bil 193 zatengwa vituo vya afya

SERIKALI imetanga zaidi ya Sh bilioni 193 kwa ajili ya kupelekea vifaa tiba katika hospitali zilizojengwa nchini kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Hayo yamesemwa leo Aprili 4, 2023 na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Dk Festo Dugange wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso lililohoji ni lini serikali itapeleka vitendea kazi na watumishi kwenye Wilaya ya Tanganyika iliyopo Mkoa wa Katavi.

Akijibu swali hilo bungeni jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki, Naibu Waziri, Dk Dugange amesema baadhi ya vituo vya afya vimeanza kupokea fedha hizo kwa ajili ya kuboresha huduma za afya.

Advertisement

Aidha, Dk Dugange amemhakikishia mbunge huyo kuwa zoezi la utoaji fedha hizo litaendelea katika Wilaya ya Tanganyika.

/* */