Sh Bil 200 kukabili mafuriko Dar

DODOMA; SERIKALI inafanya usanifu na utambuzi wa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mifereji na mito yenye urefu wa kilomita 101.15 inayokadiriwa kutumia shilingi bilioni 200 katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Saalaam.

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo na Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Tamisemi). Dk Festo Dugange alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango aliyetaka kujua kauli ya serikali kuhusu kadhia ya maji yanayotuama maeneo mengi wakati wa mvua katika jiji la Dar es Salaam.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti athari zinazotokana na mvua katika Jiji la Dar es Salaam ikiwemo kujenga kingo za mito na mifereji mikubwa yenye urefu wa kilomita 30.7 kwa thamani ya shilingi bilioni 60 kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP).

“Mheshimiwa Spika, kupitia mradi wa DMDP awamu ya pili, Serikali inafanya usanifu na utambuzi wa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mifereji na mito yenye urefu wa kilomita 101.15 inayokadiriwa kutumia shilingi bilioni 200 katika Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Saalaam.

“Mheshimiwa Spika, Vilevile, TARURA kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wanaendelea na ukamilishaji wa kazi ya ununuzi kwa ajili ya uboreshaji wa Mto Msimbazi ikiwa ni jitihada za Serikali kuendelea kukabiliana na mafuriko katika Jiji la Dar es Salaam,” amesema.

Habari Zifananazo

3 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button