DODOMA: MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere, amesema amebaini mashirika nane ya umma yalikusanya mapato ya Sh Bilioni 23.27 nje ya mfumo wa kieletroniki kwa malipo ya serikali yaani GEPG kinyume na waraka wa hazina namba 3 wa mwaka 2017.
Akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi wa serikali na Mashirika mbalimbali ya umma na binafsi, CAG Kichere amesema kushindwa kukusanya mapato kupitia GEPG kunaweza kusababisha upotevu wa mapato na kufifisha juhudi za udhibiti na uwazi katika mapato ya serikali.
“Ukaguzi umebaini kuwa halmashauri hazikukusanya kiasi cha Sh bilioni 61.15 kutoka katika vyanzo muhimu na vikubwa wakati Sh bilioni 6.
19 zilizokusanywa hazikuwasilishwa benki,” amesema Kichere
Amesema hali hiyo ina athiri uwezo wa mamlaka za serikali za mitaa kutekeleza miradi ya maendeleo na kutoa huduma bora kwa jamii.