KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu amesema serikali imedhamiria kufanya ukarabati mkubwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam ili kuufanya uwanja huo kuwa wa kisasa zaidi.
Yakubu ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2023 Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) kwa ajili ukarabati huo.
Amesema Sh Bilioni 31.3 zitatumika kukamilisha ukarabati huo katika kipindi cha miezi 12.
Aidha Katibu Mkuu amesema uwanja huo utaendelea kutumika kama kawaida hadi pale ukarabati wa eneo la kuchezea utakapoanza.