Sh bil 51 kunusuru kiwanda cha kahawa

UONGOZI wa kiwanda cha kusaga na kukoboa kahawa ya unga TANICA umewasilisha maombi ya kupata  mkopo wa riba nafuu Sh bilioni 51 kutoka Benki ya Kilimo (TADB) ili kukinusuru kiwanda hicho ambacho mitambo yake inaendelea kupoteza nguvu ya uzalishaji.

Maombi hayo yaliwasilishwa na meneja wa kiwanda hicho, Rodness Milton kufuatia ziara iliyofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera,  Alberth Chalamila  kiwandani hapo.

Milton alisema kuwa kiwanda hicho kilianzishwa mwaka 1963 na kuzindiliwa na Hayati  Mwalimu    Nyerere Kama nembo ya kutanganza kahawa ya mkoa huo bado kinaendelea na uzalishaji wa mitambo hiyo iliyosimikwa miaka 60 iliyopita.

Alisema kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa na vyama vikuu vya ushirika mkoani Kagera ambavyo ni KCU na KDCU kwa asilimia 82, serikali asilimia 10 na wadau wengine asilimia zilizobaki lakini kadri muda unavyopita ndivyo uzalishaji unavyopungua,na uwezo wa kushindana na soko unavyopotea.

Alisema kuwa awali kiwanda kilipofungililiwa kilikuwa na uwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka lakini kwa Sasa imekuwa ni ngumu kufikia tani 300 kwa mwaka Jambo ambalo limeendelea kupoteza wateja wao sokoni na kushindwa kukimbizana na wazalishaji binafsi  ambao wanamitambo ya kisasa na wanauwezo wa kuzalisha kahawa kwa haraka na Tofauti.

“Tunahitaji kunusuru kiwanda iki, kwa Sasa kiwanda hiki akiwezi kufanya kazi kwa miaka 20 ijayo, Kama tunaweza kupata Bilioni 51 tunaweza kubadilisha kila kitu,tumetuma maombi yetu serikali na wakaguzi wamekuja kukagua lakini bado hautujajibiwa, mkuu wa mkoa tunaomba utuongezee nguvu ili kunusuru ajira nyingi za watanzania ,pamoja na kahawa nzuri inayozalishwa mkoani Kagera”alisema Miltoni.

Chalamila  aliyapokea maombi hayo na kwamba atayafikisha serikalini kwani hata sasa ukarabati unaofanyika katika kiwanda icho ulitokana na ziara yake na kupeleka maombi katika wizara ya kilimo na bank ya kilimo ambao wametoa kiasi cha Sh bilioni 5  na ukarabati katika kiwanda icho unaendelea vizuri kwa sasa.

Alisema pia uongozi wa kiwanda icho uendelee kuomba kwa wahisani na wawekezaji mbalimbali  ambao wanaweza kutoa mkopo wa bilioni 51 kwa riba nafuu ambao unaweza kulipwa ndani ya miaka 30   ili kufanya haraka ya Kufunga tekinolojia ya kisasa ya kusaga na kukoboa kahawa ya unga ili kukabiliana na washindani binafsi waliopo mbele yao.

Alisema kuwa serikali tayari imefungua milango kwa wawekezaji hivyo uongozi unafursa ya kuendelea kutafuta  wawekezaji na watu wengine wa kusaidia kiwanda icho ambacho kimedumu muda mrefu ,lakini pia kuendelea kutafuta masoko mapya ndani na nje ya Afrika ili kuhakikisha kahawa inanunulika kwa wakati huku akiwawahakikishia kuwa ataendelea kuongeza nguvu ya kuomba serikalini ili msaada wa kunusuru kiwanda hicho upatikane haraka.

Habari Zifananazo

Back to top button