Sh Bil 6 zatumika kutunza vyura Marekani

TANZANIA imetumia Sh Bilion 6.69 kutunza vyura wa Bwawa la Kihansi nchini Marekani.

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere kwa mwaka 2021/2022 imebainisha kuwa vyura 500 bado wapo Marekani licha ya kumalizika kwa mkataba wa matunzo.

Serikali ilipeleka vyura hao katika bustani za Bronx na Toledo, ili kupisha ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Bwawa la Kihansi miaka 22 iliyopita kwa mkataba ulioisha mwaka 2020 na ikaongeza miaka miwili hadi mwaka 2022.

CAG Kichere amesema pamoja na kuisha kwa mkataba huo, bado hakuna taarifa za kurejeshwa kwa vyura hao nchini huku idadi yao ya sasa ikiwa haijulikani.

 

Habari Zifananazo

Back to top button