Sh bil 60 kutumika ukarabati vivuko, miundombinu

WAKALA wa ufundi na Umeme nchini (Temesa), imesema mwaka wa fedha 2022/23  inatekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa vivuko pamoja na miundombinu yake, ambapo miradi yote itatumia Sh bilioni 60.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Temesa, Lazaro Kihalahala, wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kivuko kipya cha Kisorya-Rugezi.

‘’Mwaka huu wa fedha wakala unaendelea na ujenzi wa vivuko vipya saba,  ambavyo ni Kisorya – Rugezi, Bwiro – Bukondo, Nyakalilo – Kome, Ijinga – Kahangala na Mafia – Nyamisati.

“Mikataba imeshasainiwa na wakandarasi wameshalipwa malipo ya awali na kazi inaendelea,’’ amesema Kihalahala.

Amesema miradi mingine vivuko vya Buyagu-Mbalika na Magogoni-Kigamboni ipo katika hatua za manunuzi.

 

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x