Sh Bilioni 1.6 yawekezwa mikopo ya nyumba

DAR ES SALAAM: BENKI ya Absa imeingiza hisa za Sh bilioni 1.6 kwa Taasisi ya mikopo ya nyumba ya Mortgage Refinance Tanzania Limited (TMRC)

Absa, inakua mbia wa 19 wa TMRC, ikiwa na asilimia sita ya hisa, sawa na takribani hisa milioni moja.

TMRC ni kituo cha ukwasi wa mikopo ya nyumba kinachofanya kazi nchini Tanzania, ikitoa fedha za muda mrefu kwa taasisi za fedha kwa madhumuni ya mikopo ya nyumba.

Akizungumza leo Februari 5,2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya kuikaribisha benki ya Absa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TMRC, Oscar Mgaya, aliipongeza benki na kudai kuwa amefurahishwa na namba benki kubwa za hapa nchini zinajiunga na TMRC, jambo ambalo linapanua wigo wa mikopo ya nyumba,”

Amesema hadi sasa taasisi za fedha 31 zinatoa mikopo ya nyumba nchini.

Alisema pamoja na Benki ya Absa kujiunga na TMRC, kampuni hiyo sasa ina rekodi ya uwekezaji wa jumla ya ya Sh bilioni 27.5b za wanahisa wote 19.

Nae, Mkurugenzi Mtendaji wa ABSA Obedi Laiser amesema katika kutekeleza azma yao wanatoa kipaumbele Kwa wateja wao ili wanufaike na mikopo ya nyumba.

“ABSA kujiunga kuwa wanahisa wa TMRC ina maanisha kiwango cha ufadhili wa mikopo kitaongezeka kutoka Sh bilioni 5 hadi Sh bilioni 32.

“Hii inamanaisha kuwa Absa itapata fedha zaidi ambazo zitaelekezwa kwenye mikopo ya nyumba kwa wateja wetu ili kukidhi mahitaji ya nyumba katika soko la sasa na kutatua changamoto ya uhaba wa nyumba za makazi unaokabili taifa letu,” amesema Laiser

Habari Zifananazo

Back to top button