MENEJA wa Wakala ya Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara, Mhandisi Vedastus Maribe amesema wametenga Sh bilioni 1.6 kwa lengo la kuweka taa za barabarani 308 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhandisi Maribe aliyasema hayo Novemba 8, 2023 alipozungumza na waandishi wa habari wa Kanda ya ziwa waliokuwa wakitembelea miradi mbalimbali ya kimkakati na maendeleo iliyotekelezwa na Serikali kwa fedha zake.
Mhandisi Maribe amesema Mkoa wa Mara tayari taa 900 zimekwishwa wekwa na zimechochea uchumi wa wajasriliami kwa kufanya biashara mpaka nyakati za usiku.
“Taa zimekuwa kichocheo baada ya barabara kujengwa kwa kiwango cha lami kutoka Nyamuswa kwenda Wilaya ya Bunda Kisorya na Nansio yenye urefu wa kilomita 121.9 na sehemu ya Nyamuswa kwenda Bulamba yenye urefu wa kilomita 56.4.”alisema Mhandisi Maribe
.
Mhandisi Maribe alisema matarajio yaliyopo ni kuweka taa maeneo yote yaliyochangamka na Wananchi wanafanya biashara ambapo itakuza pato la Mkoa wa Mara na mtu mmoja mmoja.
Msimamizi idara ya matengenezo kutoka Tanroads Mkoa wa Mara Mhandisi Fratern Shirima alisema kipande cha barabara kutoka Nyamuswa hadi Bunda tayari kumewekwa taa za barabarani na matarajio yaliyopo kuweka maeneo yote.
Diwani wa kata ya Nyamuswa Mganga Gayi alisema serikali imefanya kazi kubwa imebadilisha mazingira taa zinawaka usiku zimesaidia kuthibiti wahalifu nyakati za usiku na wajasiliamali kufanyabiashara hadi usiku.
Wakazi wa kata hiyo Musa Bisendo na Wazamwe Waryoba walisema uwepo wa taa umesaidia kufanya kazi mpaka saa nne usiku kabla ya kuwekwa taa walikuwa wakifanya biashara mwisho saa moja jioni.
Comments are closed.