Vyuo vya ufundi stadi kujengwa wilaya 64

SERIKALI imesema imetenga Sh bilioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo hivyo.

Akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Robert Chacha Maboto, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Juma Kipanga amesema serikali imeshakamilisha michoro na upatikanaji wa maeneo kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Akitoa ufafanuzi zaidi leo Aprili 11, 2023 bungeni Dodoma, Naibu Waziri Omary Kipanga amesema Wilaya ya Bunda ni miongoni mwa wilaya hizo ambazo zipo kwenye mpango huo.

Advertisement

Amesema Sh milioni 45 zimetolewa mwezi Machi, 2023 kwa ajili ya shughuli za awali.