Sh bilioni 11 kuboresha huduma hospitali ya rufaa Shinyanga

SERIKALI imesema itatumia Sh bilioni 11.

3 kujenga majengo ya kisasa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ili kuboresha utoaji huduma za afya.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dk Grace Magembe ametoa taarifa hiyo wakati wa makabidhiano ya eneo la ujenzi na mshauri elekezi wa masuala ya ujenzi eneo la hospitali.

Ujenzi huo unatarajiwa kuongeza majengo mapya matano, jengo la ghorofa tatu la huduma za afya ya mama na mtoto, maabara ya kisasa, jengo la kufulia nguo, jengo la dawa na jengo la kuhifadhia maiti.

Dk Magembe alikagua ujenzi jengo la nje (OPD) ambalo litatoa huduma zote za wagonjwa wa nje ikiwemo upasuaji mdogo. Jengo hilo linalojengwa na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga litagharimu Sh milioni 486 na linatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

“Haya maboresho yote yaliyofanyika hayatakuwa na tija endapo watoa huduma za afya hatutabadilika, na kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kila mtumishi analazimika kuzingatia weledi ili wananchi wafurahie huduma zinazotolewa”. amesema Dk Magembe

Habari Zifananazo

Back to top button