Sh bilioni 14.3 kuimarisha maji Kigoma Ujiji

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kigoma Ujiji (KUWASA) imepanga kukusanya na kutumia jumla ya Sh bilioni 14.3 kutekeleza shughuli mbalimbali za kutoa na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji kwa Manispaa ya Kigoma Ujiji na vitongoji vyake.

Mkurugenzi Mtendaji wa KUWASA, Poas Kilangi alisema hayo alipowasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya mamlaka hiyo na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo katika fedha hizo mamlaka inatarajia kupokea Sh bilioni 8.4 kutoka Serikali.

Kilangi alisema miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi hiki cha mwaka wa fedha ni ukarabati wa miundombinu chakavu, kuongeza mtandao wa bomba za maji katika maeneo ya Kazegunga, Kagera, Mwasenga, Businde, Kasaka, Kalalangabo na Buronge.

sG Alisema watazingatia uimarishaji wa upatiakaji huduma ya maji, kupunguza upotevu wa maji,kuimarisha makusanyo ya ankara za maji, kuboresha uwezo wa taasisi kwa kununua vitendea kazi mbalimbali, kuimarisha ubora wa maji na Kutafuta fedha ili kujenga mtandao wa kuondosha maji taka.

Akieleza kuhusu ukusanyaji huo wa mapato alisema kuwa mamlaka inatarajia kukusanya kiasi cha Sh bilioni 5.9 kutoka makusanyo ya ndani ambapo ni pamoa na mauzo ya maji kiasi cha Sh bilioni 5.6 na ada ya kuunganisha huduma ya maji kiasi cha Sh milioni 298.5.

Akifunga mkutano huo Mkuu wa Wilaya, Salum kali alisema kuwa Serikali imedhamiria kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi ikiwemo huduma ya maji safi na salama na kwamba malalamiko yote ya wananchi kwa ajili ya uboreshaji wa utoaji huduma yanafanyiwa kazi.

Habari Zifananazo

Back to top button