Sh bilioni 16 kununua magari 81

OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imetenga shilingi Bilioni 16.58 kwa ajili ya ununuzi wa magari 81 katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa.

Kati ya magari hayo, magari matano ni ya Wakuu wa Mikoa, magari mawili ni ya Makatibu Tawala wa Mikoa na magari 74 ni ya Wakuu wa Wilaya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Wizara hiyo Angela Kairuki akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha wa 2023/2024 leo April 14, 2023 Bungeni Jijini Dodoma.

Advertisement

Waziri Kairuki pia amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetengewa Shilingi Bilioni 1.

5 kwa ajili ya ununuzi wa boti nne katika Halmashauri za Wilaya za Ludewa, Buchosa, Nyasa na Sumbawanga ili kuimarisha doria, ulinzi na ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri hizo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *