Sh bilioni 19.7 kukarabati Uwanja wa Uhuru

DAR ES SALAAM: Jumla ya Sh bilioni 19.7 zitatumika kukarabati Uwanja wa Uhuru Dar es salaam ‘Shamba la bibi’, hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu @wizara_sanaatz Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa wakati wa kusaini mkataba wa kuanza kwa ukarabati wa uwanja huo leo jijini Dar es Salaam.

Ukarabati huo utafanywa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group (CRCEG) ambapo watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha miezi 12.

Uwanja wa Uhuru ni moja ya viwanja vilivyo katika mpango mkakati wa Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon 2027) ambapo Tanzania ni moja ya nchi wenyeji wa michuano hiyo mikubwa zaidi Afrika.

Advertisement

Kwa mujibu wa Msigwa uwanja huo utatumika katika mazoezi ya timu shiriki katika michuano hiyo lakini pia baada ya michuano hiyo utaupunguzia matumizi Uwanja wa Benjamini Mkapa.