Sh bilioni 2 zatolewa mkopo kwa wanawake, vijana Arusha

JIJI la Arusha limetoa mikopo ya asilimia kumi ya Sh bilioni 2.656 kwa vikundi 169 kwaajili ya makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kusisitizwa kuwa wabunifu zaidi

Aidha watu wenye ulemavu wanaruhusiwa kukopa mikopo hiyo bila kuwa na kikundi na dirisha lipo wazi na kusisitiza Jiji litaendelea kutoa mikopo kwa njia ya mtandao ili kupata takwimu sahihi za wanufaika.

Advertisement

Akishuhudia zoezi la utoaji mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtahengerwa amesisitiza wanaopewa mikopo kuwa wafanyabiashara wenye ubunifu na kuacha biashara za mazoea.

Dc Mtahengerwa amesema endapo wapewaji mikopo hiyo wakiwa wabunifu wataongeza tija katika biashara zao ikiwemo kufungua fursa za kutangazabiashara zao ili kupata soko la ndani na hata nje ya mkoa wa Arusha

Pia uombaji mikopo kwa njia ya kieletroniki (mtandao ) ni mzuri kwani unaonyesha vikundi vingapi vimepata mikopo na vipo wapi hivyo Jiji litaendelea kutoa mikopo kwanjia hiyo ili kujua makundi yaliyofikiwa katika utoaji na ujeshwaji wa mikopo na alimshukuru Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuwakwamua wananchi katika hali ya chini na kufungua fursa za kibiashara.

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,Hargeney Chitukuro amesena haijapata kutokea Jiji kutoa mikopo na kusisitiza kuwa mikopo hiyo itaenda kwa vikundi saba ikiwemo viwanda vidogo,28 wasafirishaji,77 wakulima na wafugaji na vikundi 169 vya kada mbalimbali ikiwemo wanawake,walemavu na vijana

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *