Sh bilioni 30.39 zafidia wananchi bomba la mafuta

SERIKALI imeeleza kuwa Sh bilioni 30.39 zimetolewa kwa wananchi 7,486 kati ya 9,122 katika eneo la Mkuza ili kupisha ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) lenye urefu wa km 1,443.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma leo, Majaliwa amesema serikali imeendelea kulipa hisa za umiliki katika Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki hadi kufikia Dola milioni 131.0.

Amesema tayari kibali cha kuanza ujenzi kimetolewa Januari 2023. Sambamba na ujenzi wa karakana ya kuweka mfumo wa kupasha joto mabomba.

Habari Zifananazo

Back to top button