WAKALA wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Mara imeanza matengenezo ya barabara ya Sanzate kupitia Nata hadi Mugumu yenye urefu wa kilomita 126.73 kwa kutumia zaidi ya Sh bilioni 39
Meneja wa Tanroads mkoa huo, Mhandisi Vedastus Maribe ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa Kanda ya Ziwa waliotembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya kimkakati iliyotumia fedha za ndani.
Mhandisi Maribe amesema barabara hiyo ilianza kutengenezwa mwaka 2020 itakuwa kwa kiwango cha lami pia sasa imefikia asilimia 41 ya ujenzi na pindi ikikamilika itakuza uchumi kwa wananchi wa mkoa huu.
“Barabara hii ni kiungo muhimu Kati ya wilaya ya Musoma,Butisma na Serengeti na itakapo kamilika hata mikoa jirani itanufaika na Ile ya mali itafahisishiwa kwenye Shughuli za utalii katika mbuga za wanyama Serengeti. “amesema Mhandisi Maribe.
Pia Mhandisi Maribe amesema barabara ya Tarime kwenda Mugumu yenye urefu wa kilomita 87.14 na Mogabiri kwenda Nyamongo yenye urefu wa kilomita 25 itajengwa kwa kiwango cha lami.
“Ambapo vipande hivyo vya Barabara vitagharimu zaidi ya Sh billioni 34 ulianza mwaka 2022 na kutarajia kukamilika mwaka 2024 Fedha hizo zimetolewa na serikali kwa asilimia 100 na wakandarasi wanaotekeleza kazi hiyo na Watanzania.”amesema Mhandisi Maribe.
Comments are closed.