Sh bilioni 6.4 kuleta maji wilaya tatu Shinyanga

WAKALA wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoani Shinyanga imewasainisha wakandarasi mikataba saba ya miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 6.4 itakayotekeleza wilaya tatu za Shinyanga, Kishapu na Kahama.

Ambapo mikataba sita ni miradi ya maji ambayo itatekelezwa kwa kipindi tofauti huku mkataba mmoja ukiwa wa ununuzi wa mabomba na viungio.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya utilianaji saini wa mikataba hiyo ambapo amesema wakandarasi wanatakiwa waheshimu mikataba

RC Mndeme amesema wakandarasi wanatakiwa kuwa waaminifu kwani baadhi yao wamekuwa wakitumia mabomba yasiyoendana na uhalisia nakufanya yapasuke nakuhatarisha afya za watumiaji.

Amesema Mkoa wa Shinyanga una vijiji 506 ikiwa vijiji 58 tu ndiyo havina maji ambapo wananchi wake wanatumia maji kutoka vijiji jirani vyenye mabomba huku Serikali ikiendelea kutatua changamoto hiyo.

“Mkoa kwa Sasa una asilimia 66 ya upatikanaji wa maji vijijini na kufikia mwaka 2025 itafikia asilimia 85 Kama ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020 Hadi 2025 unavyoeleza.”amesema Mndeme.

Meneja wa Ruwasa Shinyanga, Mhandisi Juliette Payovela amesema mwaka uliopita walitumia Sh bilioni 28.9 katika utekelezaji wa miradi ya maji 33 pia kuna vyombo vya watumia maji (CBWSO) 29 ambavyo vimefundishwa utumiaji wa mifumo ya Kielektroniki katika ukusanyaji wa fedha.

“Leo tunasainishana mikataba saba ambapo wakandarasi kila mmoja atasaini kwenye eneo lake nakuhakikisha kazi inafanyika kwa wakati.”amesema Mhandisi Payovela.

Mkandarasi Stephene Owawa kutoka kampuni ya Geo-Spatia Classic Works LTD kwa niaba ya wakandarasi amesema hawataiangusha Serikali watatekeleza vizuri kwa mujibu wa mikatabaunavyoeleza hivyo waondoe wasiwasi.

Habari Zifananazo

Back to top button