Sh bilioni 6 kunufaisha vijiji 13 mradi wa maji Kishapu

WAKAZI 49,965 kutoka vijiji 13 vya kata tatu vya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga watanufaika na mradi wa maji wa Ziwa Victoria uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 6.6.

Hayo yalisemwa jana na meneja wa Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima wakati wa ziara ya wajumbe wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyang wakiongozwa na mbunge wa Viti Maalum Santiel Chilumba.

Advertisement

Mhandisi Kamazima alisema mradi huo unatekelezwa kwa fedha za serikali na mkandarasi amelipwa malipo ya awali huku akivitaja vijiji vitakavyo nufaika kuwa ni Igaga A na B, Isagala, Mwamashele, Busongo, Mwamanota, Bubinza, Lwagalalo, Mwamadulu,Nyawa,Beledi,,Lagana na Mihama.

“Utakapokamilika mradi huo utawapunguzia muda wa kufuata maji umbali mrefu na kuwaongezea muda wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii pia kupunguza mlipuko wa magonjwa yatokanayo na kutumia maji yasiyo safi na salama.”alisema Kamazima.

Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Aisha Kitandala alisema lengo la chama kuona wanawake wanatatuliwa kero zao hasa upande wa maji ambao ulikuwa ukionekana ukosefu wa maji ni chanzo cha ukatili kwa wanawake nakuwashauri Ruwasa kutumia vibarua wanatoka kwenye eneo hilo ili wanufaike.

Mbunge viti maalum Santiel Chilumba ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ziara hiyo alisema kero kubwa ilikuwa ni maji na kipindi cha miaka miwili ya Rais Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kwenye miradi ya maji lengo kuondoa kero hiyo kwa wananchi na wananchi waisimamie vizuri kwani miradi inatakiwa kuwa endelevu.

“Mradi huu ni mkubwa kwa mkoa mzima wa Shinyanga kwa kutumia fedha nyingi na hatutaki Rais akwamishwe ila tunaipongeza Ruwasa ndani ya mkoa huu haijamkwamisha Rais ipo bega kwa bega”alisema Chilumba.

Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo alisema ilani ya chama cha Mapinduzi waliyokuwa wakiinadi imetekelezwa vizuri kwa kumtua mama ndoo kichwani kwa vijiji hivyo kwani kilio kikubwa kwa wananchi wa vijiji hivyo ilikuwa ni kupata huduma ya maji.

Diwani wa kata ya Lagana Luhende Sana alisema kata yake ina vijiji vitano ambavyo vyote vitanufaika kwani awali walikuwa wakinunua maji ndoo moja sh 1000 au kufuata umbali wa kilomita tano mto tungu.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *