Sh bilioni 65 zahitajika athari za mvua

DAR ES SALAAM: Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), imesema inahitaji Sh bilioni 65.100 ikiwa ni fedha ya dharura kwa ajili ya ukarabati wa barabara na madaraja yaliyoharibika kwa mvua.

Mtendaji Mkuu wa Tarura Mhandisi Victor Seif ameyasema hayo leo Januari 24, 2024 katika katika kikao kazi na menejimenti ya Tarura, makatibu tawala wasaidizi miundombinu, makandarasi wazawa, wataalamu washauri na taasisi za kibenki, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akitoa mchanganuo wa fedha hizo amesema tathmini ya uharibiu wa miundombinu ya barabara uliosababishwa na mvua imefanyika kuanzia mwezi Juni 2023 hadi Desemba 2023 ikijumuisha halmashauri 184.

Amesema tathmini hiyo inaonesha kuwa kiasi cha zaidi ya sh bilioni 33.

124 zinahitajika kwa ajili ya marekebisho ya miundombinu ya barabara iliyoathirika na mvua kwenye halmashauri 153.

Aidha amesema, inakisiwa jumla ya sh bilioni 32 zinahitajika kati ya Januari hadi Juni 2024 ikiwa ni fedha za tahadhari kwa ajili ya uharibifu wa mvua hadi msimu utakapoisha mwezi Juni, 2024.

“Hivyo kulingana na tathmini hiyo na makisio hadi msimu wa mvua utakapoisha jumla ya Sh bilioni 65.100 zinahitajika kama fedha za tahadhari, kwa kuwa sh bilioni 21.460 zimeshatengwa kutakuwa na nakisi ya sh bilioni 42.640,” amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button