SERIKALI imetoa jumla ya Sh bilioni 762.
99 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR).
Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.
Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma, Majaliwa amesema kipande cha Dar es Salaam kwenda Morogoro (km 300) utekelezaji wake umefikia asilimia 97.91 na kipande cha Morogoro kwenda Makutupora (km 422) umefikia asilimia 92.23.
Majaliwa amesema kipande cha Mwanza – Isaka (km 341) umefikia asilimia 25.75 na kipande cha Makutupora -Tabora (km 371)umefikia asilimia 4.
59 na kuanza kwa ujenzi wa kipande cha Tabora – Isaka (km 165) na Tabora – Kigoma (Km 506).