Sh bilioni 77. 23 kuendeleza ujenzi uwanja wa ndege Msalato

SERIKALI imetoa Sh bilioni 77.23 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Msalato ambapo utekelezaji umefikia asilimia 10.2.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma leo, Majaliwa amesema kazi nyingine ni kukamilika kwa upanuzi wa njia ya kutua na kuruka ndege na kufungwa kwa mfumo wa kuongozea ndege katika Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.

Advertisement

Amesema kukamilika kwa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Geita na kuendelea na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Songea kwa asilimia 98, Iringa asilimia 42 na Musoma asilimia 43.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *