Sh bilioni 869 kutekeleza JNHPP

SERIKALI imetoa jumla ya Sh bilioni 869.93 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere utakaozalisha Megawati 2,115. Mradi huo umefikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwasilisha mapitio na mwelekeo wa kazi za serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024.

Akizungumza leo bungeni jijini Dodoma leo, Majaliwa amesema hadi Februari, 2023 kiwango cha maji kimefikia mita 134.39 kutoka usawa wa bahari ikilinganishwa na kiwango cha mita 163 kinachohitajika ili kuanza uzalishaji.

Advertisement

Zoezi la ujazaji maji katika bwawa la kufua umeme wa maji katika mradi huo lilizinduliwa rasmi na Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Desemba 2022.