Sh bilioni 92 kujenga barabara Bugene-Burigi Chato

SERIKALI imetoa Sh bilioni 92.84 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Bugene kwenda Burigi Chato Hifadhi ya Taifa yenye urefu wa kilomita 60 na kipande cha Bugene kwenda Kasulo hadi Kumunanzi yenye urefu wa kilomita 128.5 katika Mkoa wa Kagera.

Kaimu Meneja wa Wakala ya  Barabara nchini (TANROADS) mkoa huo ametoa taarifa hiyo Novemba 11, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea mradi huo inayotekelezwa na mkandarasi kutoka kampuni ya China CCECC.

Mhandisi Mwaikokesya alisema ujenzi wa barabara hizo umeanza utekelezaji na kufikia asilimia 27.7 ikiwa kipande cha kilomita moja kilichopo kwenye Mlima wa Nyaishozi kimeanza kupasuliwa miamba na kuchimba kina kwa kwenda chini ya ardhi na kufikia mita 26.

Mhandisi Mwaikokesya alisema ujenzi unatarajia kukamilika Novemba 2024 ikiwa usanifu ulifanyika mwezi Februari 2022 na kampuni hiyo kusaini.

“Lengo la kuiboresha zaidi eneo la mlima ilikuwa changamoto kubwa magari yalikuwa yanaanguka kila siku wakati mwingine kukwama hadi siku mbili Serikali ikaona kutatua changamoto hii.”alisema Mwaikokesya.

Aidha mhandisi Mwaikokesya alisema kuanza kwa ujenzi huo umeweza kutoa fursa kwa vijana ikiwa tayari ajira za muda 279 zimetolewa na Wananchi wa Wilaya ya Karagwe wananufaika kwa ajira.

Mhandisi Mwaikokesya alisema barabara hiyo ni kiwango cha udongo ambapo inawekewa kiwango cha lami ili wakulima waweze kusafirisha ndizi kwenda sokoni bila kukwama njiani.

Kaimu mhandisi Mshauri mkazi Onesmo Mgoha alisema maendeleo ya mradi huo yako vizuri hivyo wanao uhakika wakumaliza kwa wakati mvua sio kikwazo kwao watajitahidi kutumia njia mbadala ikiwemo kuongeza masaa ya kazi.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Eviessity
Eviessity
20 days ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 20 days ago by Eviessity
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x