Sh Mil 200 zatengwa miundombinu mabweni

DODOMA; SERIKALI imesema mwaka 2023/2024, imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mabweni, ili kuunga jitihada zilizofanywa na wananchi za kujiletea maendeleo.

Pia imesema imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na katika mwaka wa fedha wa 2022/23, Serikali iliidhinisha kiasi cha Shilingi Bilioni 9.21 kwa ajili ya ukamilishaji wa mabweni 461, kati ya hayo mabweni 28 ni kwa ajili ya shule za msingi zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum.

Kauli hiyo imetolewa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Regina Ndege Qwaray aliyehoji ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa mabweni yaliyoanzishwa na wananchi kwa michango yao katika shule za kata nchini

“Kwa Mwaka 2023/2024, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi Milioni 200 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mabweni, ili kuunga jitihada zilizofanywa na wananchi za kujiletea maendeleo.

“Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mabweni kila mwaka kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button