‘Sh mil 5 kila goli ni mechi zote CAF’

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema ahadi ya kununua magoli yatakayofungwa na Simba SC na Yanga kwenye mashindano ya kimataifa iliyowekwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea hadi mwisho wa mashindano ambayo timu hizo zinashiriki.

Msigwa amesema katika michezo ya timu hizo iliyobaki kabla ya mashindano kumalizika, kila timu itaendelea kupata Shilingi milioni 5 kwa kila goli.Simba na Yanga kila moja imebakisha michezo minne hatua ya makundi katika michuano inayoandaliwa na Shirikisho la mpira wa Miguu Afrika (CAF).

Yanga SC iliondoka na Sh milioni 15 baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe juzi Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam katika Kombe la Shirikisho, huku Simba ikipoteza kwa kufungwa mabao 0-3 na Raja Casablanca uwanja huo huo Ligi ya Mabingwa Afrika.

Habari Zifananazo

Back to top button