Sh mil 72 zafidia mitaa 15 Bunda

DODOMA: KATIKA mwaka wa fedha 2023/2024 serikali imekwishalipa zaidi ya Sh milioni 72 kwa wahanga 299 kwa takriban mitaa 15 ya Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Haya yamebainishwa leo Mei 23, 2024 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Dunstan Kitandula wakati akijibu swali la Robert Chacha Maboto aliyetaka kujua Serikali italipa lini kifuta jasho/machozi kwa wahanga wa wanyama waharibifu kwa Wananchi wa Bunda mjini.

Soma pia: https://habarileo.co.tz/mali-ziuzwe-kufidia-waliopigana-vita-ya-dunia/

Kitandula amesema kuwa wananchi wa Wwilaya hiyo ambao wamekuwa wakipata changamoto ya uharibifu unaofanywa na wanyamapori wakali na waharibifu wamekuwa wakilipwa kifuta jasho/machozi kwa nyakati tofauti tofauti kadri fedha zinavyopatikana.

Pia, naibu waziri ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kushughulikia madai mengine ya wananchi 1,111 kutoka katika Halmashauri ya Mji wa Bunda ambayo yamekwishawasilishwa wizarani. Malipo yatafanyika mara tu baada ya taratibu kukamilika.

Soma pia: https://www.instagram.com/p/C7TcOGTM1qv/?utm_source=ig_web_copy_link&igsh=MzRlODBiNWFlZA==

Katika hatua nyingine, Kitandula amesema kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii inahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa maafisa wanyamapori waliopo kwenye halmashauri za wilaya kwa kuwa madai ya kifuta jasho na machozi huanzia kwao na pale ambapo wanakuwa wamechelewesha hufanya madai hayo kuchelewa kulipwa.

Habari Zifananazo

Back to top button