Sh milioni 100 kukamilisha Zahanati Kilindi

DODOMA: SERIKALI imepanga kutumia fedha za makusanyo ya ndani kiasi cha sh millioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Masagalu kilichopo katika Halmashauri ya Kilindi.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya Wabunge yanayohusu sekta ya afya wakati wa kikao cha kwanza cha Bunge la 13 lililoanza leo jijini Dodoma.

Dugange amesisitiza kuwa Serikali imeshaanza mchakato wa kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa Kituo cha Afya cha Loliondo ili kuondoa adha ya wananchi wa eneo hilo kukosa huduma pindi wanapohitaji huduma za afya.

“Kituo cha Afya cha Loliondo ni miongoni mwa vituo 199 ambavyo Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeviainisha na kuviweka kwenye mpango wa ukarabati na tayari Serikali imeanza kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi”, amesema Dugange.

Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha fedha inapatikana kwa wakati ili kukamilisha ukarabati na upanuzi wa vituo vya afya ikiwa ni pamoja na kukamilisha maboma katika zahanati zote nchini.

Habari Zifananazo

Back to top button