Sh milioni 100 za halmashauri zanufaisha vikundi 13 vya wanawake

MANISPAA ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imekabidhi mfano wa hundi yenye thamani zaidi ya Sh milioni 100 kwa vikundi 13 vya wanawake wajasiliamali ikiwa ni mkopo kutoka kwenye asilimia 4 inayotokana na mapato ya ndani ya halmashauri.

Akizungumza leo Machi 7, 2023 mkoani hapa kuelelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani kesho, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Hanafi Msabaha amesema wanawake hao wakati wanapotafakari usawa wa kijinsia kati wa Mwanamke na Mwanaume wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanakuwa vizuri kiuchumi.

DC Msabaha ameipongeza Manispaa hiyo kwa jitihada mbalimbali zinazofanyika kwa wanawake ikiwemo hatua ya kuendelea kutenga mikopo kwenye asilimia 10 ambayo ipo kisheria kwa sasa hivyo amesisitiza kwamba waendelee kuwakopesha akina mama hao ili waweze kujikwamua kiuchmi.

“Vikundi hivi tutaendelea navyo na taasisi za kifedha pia endeleeni kuwasaidia akina mama, endeleeni kuwapa elimu ya kiuchumi na ya kibiashara na endeleeni kufikiria mmpate nzuri zaidi ya mikopo hii ya akina mama ambao inaweza ikawa na riba ndogo kuliko sasa”. Amesema Msabaha.

Aidha, Manispaa imekabidhi mahitaji mbalimbali kwa Jamii yaliyotolewa na makundi mbalimbali ya kijamii kutoka kwenye manispaa hiyo ikiwemo vifaa tiba ambavyo vitaenda kusaidia utoaji wa huduma katika zahanati ndani ya manispaa, uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi na mengine.

Ofisa Maendeleo ya Jamii katika Manispaa hiyo, Juliana Manyama amesema shughuli hizo za maadhimisho na utoaji wa huduma mbalimbali ambazo zimefanyika katika siku hizo zote za maadhimisho kuanzia Machi 1, mpaka sasa wanapoelekea kilele chake Machi 8, 2023 zimefanywa na Wanawake wa Manispaa kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuweza kufanikisha siku hiyo pekee na muhimu kwao.

Habari Zifananazo

Back to top button