Sh milioni 190 kusaidia watoto njiti

TAKRIBANI Sh milioni 190 zimekusanywa kutoka Taasisi ya Hisani ‘Samakiba’ na Dorris Mollel kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya watoto waliozaliwa kabla ya muda yaani ‘njiti.

Tamasha la Samakiba kilele chake litakuwa Juni 20 mwaka huu katika uwanja wa Azam Complex,  Chamazi ambapo kutakuwa na mechi za mpira wa miguu na tamasha la muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 19, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi,  Dorris Molle amesema fedha hizo zimekusanywa kutoka katika taasisi mbalimbali zitakazotumika kupunguza vifo kwa watoto njiti katika Hospitali ya Kibiti Mkoa wa Pwani na Hospitali ya Mkoa wa Kigoma.

Advertisement

Amesema kwa mujibu wa takwimu iliyotolewa na mamlaka husika ni  asilimia 48 ya watoto wachanga wanaozaliwa na kufa, wengi wao wanakuwa ni watoto waliozaliwa kabla ya muda.

Doris amesema fedha hizo pia zimegawanyika katika kusaidia changamoto zingine kama tauro za kike, madawati, gesi pamoja na vifaa tiba ili kusaidia serikali na Jamii katika kukabiliana na changamoto hizo.

“Tumekuwa tukishirikiana kwa vitu vingi, lakini nikiwa kama miongoni mwa mtoto niliyezaliwa njiti, nami nafanya hivi kama kurudisha shukrani kwa Jamii” amesema Doris.

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ambaye ni mkurugenzi mwenza wa taasisi ya  Samakiba  amesema wamekuwa wakifanya kazi ya kuisaidia jamii kupitia taasisi hiyo kwa miaka saba.

Amesema kikubwa wamekuwa wakitumia majina yao katika kuisaidia jamii kupitia vipaji vyao na uwezo wao.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *