Sh milioni 20 kujenga ofisi ya CCM Mbogwe

MKUU wa WIilaya ya Mbogwe, Sakina Mohamed amekusanya jumla ya Sh milioni 20 kwa ajilii ya ujenzi ya ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo.

Sakina amekusanya fedha hizo leo Desemba 9,2023 katika harambee aliyoiendesha kwa wadau wa chama hicho.

Akizungumza Sakina amesema atasimama imara kuhakikisha CCM wilayani Mbogwe inakamilisha ujenzi wa ofisi yake.

Advertisement

Amesema yeye kama Kamisaa wa chama hafurahishwi kuona CCM wlayani humo haina ofisi inayotafsiri heshima ya Chama hicho na kwa kuwa Rais aliyemteua ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM hawezi kufurahishwa akifika Mbogwe na asipate ofisi yenye hadhi.

Amesema ofisi hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu Sh milioni 45.

1 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *