Sh milioni 5 atakayempata mwanafunzi aliyepotea

MKUU wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera, ametangaza dau la Sh milioni tano kwa yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa mwanafuunzi wa kidato cha tano Esther Noah Mwanyilu.

Esthet alikuwa mwanafunzi katika shule ya Sekondari ya Pandahill aliyetoweka shuleni Mei 18, 2023.

“Tunaomba wananchi watoe ushirikiano, yeyote atakayefanikisha kupatikana kwa binti huyu, atapata asante ya Sh milioni tano,”amesisitiza Homera na kuongeza kuwa kupotea kwa mtoto huyo ni maumivu makubwa kwa familia.

“Kupotea kwa mtoto huyu ni maumivu makubwa kwa familia yake, chukulia mtoto wako amepotea na hajulikani alipo utajisikiaje? Sisi ni viongozi lakini ni wazazi pia tunajisikia maumivu sana na leo tutakuwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa ili kujua tumefika hatua gani,” amesema.

Amesema atawasilisha taarifa kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alitoa maagizo ya kufanyika uchunguzi zaidi kuhusu kupotea kwa mwanafunzi huyo.

“Jitihada mbalimbali zilifanyika ikiwa na pamoja na kuwahoji walimu wa shule, wanafunzi, marafiki wa Ester na jumbe zote alizokuwa akiandika zilizoachwa na mwanafunzi huyo zimechukuliwa na kupelekwa kwenye maabara kwa ajili ya uchunguzi ili kubaini kama ni jumbe za mwanafunzi huyo aliandika mwenyewe au laah,” amesema.

Naye, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema juhudi za kumtafuta zinaendelea ikiwa ni pamoja na kuwahoji wale wote aliwataja kwenye ujumbe aliocha kabla ya kuondoka.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button