Sh milioni 800 kuboresha majengo hospitali Lushoto

TANGA: Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zaidi ya Sh milioni 800 kuboresha baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.

MKUU wa Wilaya ya Lushoto, Japhari Kubecha ametoa taarifa hiyo jana alipofanya ziara katika ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Akitoa taarifa kuhusu matokeo ya ziara yake, DC Kubecha amesema ifikapo Juni 30 mwaka huu, itakuwa mwisho wa maboresho hayo.

“Tutafika kukagua na kujionea thamani ya fedha ambayo Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuwapenda wananchi wa Lushoto ameleta fedha hiyo,” amesema DC Kubecha.

Katika ziara hiyo DC Kubecha aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo na wengine.

Habari Zifananazo

Back to top button