Sh tri 1.15 kujenga madarasa msingi, sekondari

‘Wenye mapenzi na uandishi wakasome’

SERIKALI inatarajia kutumia jumla ya Sh  Tril. 1.15 kujenga madarasa kwenye shule za msingi na sekondari kote nchini, ikiwa ni kuhakikisha miundombinu sekta ya elimu inazidi kuimarika

Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Januari 15 jijini Dodoma akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni muendelezo wake wa Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Serikali.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeboresha sana sekta ya elimu kuanzia elimu ya msingi mpaka elimu ya Juu.

Advertisement

“Mhe. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuangalia kwa karibu sekta ya elimu kwa sababu hapa ndipo kuna Watanzania tunaowaandaa na sasa tumeandaa mradi mkubwa unaitwa BOOST. Huu mradi ni kishindo kingine kikubwa kwenye sekta ya elimu.

“Tunataka kuja kujenga madarasa kwenye shule za Msingi na Sekondari.

Mradi huu utakuwa wa miaka 5 na unatarajiwa kuanza mwaka huu 2023 na mwaka huu kwa kuanzia zimetengwa Sh Bil.250.9 ambazo zitajengwa madarasa 9,000 kwa ajili ya shule za msingi na awali,” amesema Msigwa.

Ameongeza kuwa mradi huo utaenda kumaliza kabisa tatizo la msongamano wa wanafunzi katika shule za msingi nchini.