Sh tri.121 zaokolewa matumizi gesi asilia

SERIKALI imeokoa kiasi cha shilingi trilioni 121, sawa na dola za Marekani bilioni 52 tangu kuanza kutumia nishati ya gesi asilia kuzalisha umeme nchini mwaka 2004.

Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA), Mhandisi Charles Sangweni amesema kwa sasa gesi asilia inachangia asilimia 70 upatikanaji wa umeme nchini.

Mhandisi Sangweni ameeleza hayo wakati wa ziara ya bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka hiyo, wajumbe wa kamati za bodi, menejimenti ya PURA na baadhi ya wataalamu wa mamlaka hiyo waliotembelea eneo uchimbaji wa gesi asilia,  Ntorya, mkoani Mtwara.

Amesema kabla ya kuanza kutumia gesi, uzalishaji wa umeme nchini uliigharimu serikali fedha nyingi kununua nishati ya mtafuta.

Amesema iwapo serikali itaendelea kuwekeza zaidi kwenye miundombinu ya usafirishaji wa gesi, itawezesha nishati hiyo kufika na kutumika maeneo mengi na kuendelea kuokoa fedha nyingi, ambazo zitatumika kwenye matumizi mengine kwa manufaa ya taifa.

“Gesi ili ifike sehemu nyingi na kutumika ni lazima ujenge miundombinu na ndio maana mwaka 2013 hadi 2015 tulijenga bomba kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam, kwa hiyo ni suala la serikali kuwekeza zaidi kwenye miundombinu,” amesema.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x