Sh Trilioni 1 kibindoni sekta ya madini

DAR ES SALAAM: Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi  wa Rais Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Madini imekusanya  Sh Trilioni 1.9  kutoka katika  vyanzo mbali mbali ikiwemo ada za leseni, ada za ukaguzi za kijiolojia, mrabaha na faini mbali mbali.
Hayo yamesemwa leo Machi 14, 2024 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akielezea mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Samia, aliyeingia madarakani  rasmi Machi 2021.
Mavunde amesema, mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka  hadi kufikia asilimia 9.1 mwaka 2022.
Aidha, amesema katika kipindi cha muda mfupi wa kati cha robo ya tatu Julai hadi  Septemba   mwaka 2023 sekta ilichangia asilimia 10.4 ikilinganishwa na mchango wa asilimia 9.5 katika kipindi kama hicho mwaka 2022.
“Mwenendo huu wa mchango unaakisi dhamira ya serikali kuhakikisha sekta hii inaimarika na kuweza kuchangia hadi asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025,” amesema Mavunde
Amesema, katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024, Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kusimamia biashara ya madini katika masoko ya madini hapa nchi ili kuhakikisha yanafanya kazi kwa ufanisi.
” Katika kipindi rejewa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini zimeendelea kuongezeka ambapo jumla ya masoko 42 na vituo vya ununuzi wa madini 100 vimeanzishwa nchini, “amesema Mavunde
Pia, amesema katika kipindi cha mwezi Machi, 2021 hadi Februari, 2024 kiasi cha tani 52.9 za madini ya dhahabu, tani 1,204.83 za madini ya Bati, karati 54,025.89 za madini ya Almasi,
karati 183,551.87 na tani 121.34 za madini ya tanzanite na kiasi cha karati 171,286.92 na tani 94,647.94 za madini mengine ya vito yaliuzwa katika masoko ya madini.
Amesema mauzo hayo ya madini
yamechangia makusanyo kutoka kwenye mrabaha na ada ya ukaguzi kiasi cha Sh Bilioni 476.78.

Habari Zifananazo

Back to top button