Sh trilioni 280 zatakatishwa- Mpina

Ahoji Mwigulu kibali kapata wapi?

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina ameichambua taarifa iliyowasilishwa bungeni kuhusu usalama wa kifedha ‘Financial Intellegence Unit’ (FIU) ambayo inaonyesha zaidi ya sh trilioni 280 zimetakatishwa.

Akichangia bajeti kuu ya serikali leo Juni 20, 2023 Mpina amesema utakatishaji wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi, na ufadhili wa silaha za maangamizi, taarifa ya FIU (financial intelligence unit) inaonyesha fedha taslimu na zile zilizopitia kwenye miamala ya simu zaidi ya sh trillion 280 hadi Aprili 25 mwaka huu ni haramu.

Alihoji “hivi utawezaje kukusanya fedha katika nchi ambayo ina fedha haramu zaidi ya sh trilioni 280?

“Alafu huoni mikakati ya kushughulika na hizi fedha, hauoni mikakati ya FIU kushughulika na hizi kesi, na katika kipindi hicho kesi zilizosikilizwa au miamala iliyochambuliwa na FIU ni miamala 769 tu kati ya miamala 16,035…;

“Maana yake kuna ukwepaji wa kodi uliopitiliza, kuna ‘financial cash flow’ ‘utoroshaji wa fedha nje ya nchi nyingi’ uliyopitiliza, kuna ‘transfer financial un illegal’ zilizopitiliza utakusanyaje kodi katika mazingira kama hayo?

“FIU ni kitengo tu ambacho hakina mechanism (mikakati) yoyote, DCI (Mkurugezi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai) anashughulikaje, PCCB (Taasisi ya kupambana na rushwa) anashughulikaje, DPP anashughulikaje? (Mkurugenzi wa Mashtaka) Kuhakikisha hii miamala tunapata fedha.

“ECF (Extended Credit Facility), LTP (Last Traded Price) mikopo imeingiwa na serikali Sh trilioni 2.75.

“Kamati imetueleza hapa zaidi ya sh trilioni 2.75 zilikwenda kwenye matumizi yasiyo na tija. Tumekuwa tukiambiwa tunakopa fedha inakwenda kwenye miradi ya maendeleo, leo kamati ya bajeti inaprove kuwa fedha hizi zinakopwa na nyingi haziendi kwenye miradi kama tunavyoelezwa.

“Leo deni la taifa limekuwa kwa asilimia 13.9 ni almost asilimia 14.9 kutoka mwaka mmoja kwenda mwaka mwingine, mikopo ambayo hatujawahi kukopa kwa kiwango hicho. Lakini tukiambiwa tumekopa kwa kuwa tunaipeleka kwenye miradi ya kimkakati.

“Tuna ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo inaeleza zaidi ya sh trilioni 1.285 zimekopwa nje ya kibali cha bunge katika mwaka husika wa fedha, sasa mikopo kama hii ikiendelea kuruhusiwa, bunge hili likiendelea kuruhusu mambo haya yafanyike, na mikopo hii ya ECF na LTP ambayo hata bunge ilielekeza mkajadiliane, na nimeona katika majadiliano mmeshindana.

“Leteni jedwali zima linaloonyesha sh trilioni 2.75 zinaenda kwenye maeneo gani, na Waziri wa fedha (Mwigulu Nchemba) amepata kibali wapi cha kwenda kuhidhinisha mikopo ya matumizi ya kawaida, wakati msimamo wa nchi fedha zote zinakopwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

“EPC PLUS F (Engineering Procurement Construction and Financing) Mikopo mingine mfadhili anakuja na fedha, anaajiri wakandarasi yeye, anasimamia mradi yeye, anafanya ‘design’ yeye, ananunua yeye, mbona hatupewi maelezo ya kina taifa litapata faida gani?

“Tutasimamieje gharama, tutasimamiaje ubora kwa wakandarasi ambao hatuwalipi sisi? Lakini pia mikopo hiyo ni ndani ya mikopo yetu tunayokopa au ni mikopo mingine? Alihoji Mpina

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button