‘Sheria ipo kuzuia uvutaji sigara hadharani’

DODOMA: WIZARA ya Afya imesema tayari bunge limepitisha Sheria ya Udhibiti wa Tumbaku ijulikanayo kama “The Tobacco Products (Regulation) Act, 2003” ambayo imetoa katazo la uvutaji wa Sigara hadharani.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amebainisha hayo leo Aprili 30,2024 Jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Tumbe, Amour Khamis Mbarouk aliyeuliza Je, ni lini Serikali italeta Sheria ya Kuzuia uvutaji wa sigara na mazao mengine hadharani.

Aidha amesema sheria hiyo imezuia matangazo ya tumbaku na bidhaa zitokanazo na tumbaku kwenye maeneo ya umma ikiwemo vyombo vya habari, billboards na kwenye matamasha mbalimbali.

Vile vile Dk Mollel ametoa wito kwa Wabunge kuwa mabalozi wa udhibiti wa Tumbaku katika jamii ili kusaidia wananchi kuepuka magonjwa yasiyoyakuambukiza.

Habari Zifananazo

Back to top button