Sheria kali zahitajika kulinda viumbe wa majini

DAR ES SALAAM: Sheria kali inapaswa kuwekwa ili kuzuia uvuvi wa viumbe vya majini ambavyo vipo kwenye hatari ya kupotea ili kuvinusuru.

Viumbe hao ni jongoo bahari, nguva, kisukuku na kasa.

Ofisa Mwandamizi wa Uvuvi kutoka Soko la Kimataifa la Samaki Feri mkoani Dar es Salaam, Ramadhani Mtabika amesema hayo alipozungumza na HabariLeo.

Amesema viumbe hao ambao wako kwenye hatari ya kupotea kwa mujibu wa sheria za nchi na za kimataifa hawaruhusiwi kuvuliwa.

Amesema changamoto iliyopo katika sheria hiyo ni kuwepo kwa adhabu ndogo ambayo haikomeshi uvunaji wa hao viumbe wa baharini ambao wako kwenye hatari ya kupotea.

“Mfano kwa kasa ukikamatwa faini ni shilingi 200,000 mpaka shilingi milioni moja, na haisemi kwa kasa wangapi.

“Kukomesha uvunaji huo inahitaji kufanywa mapitio ya kanuni ili iwekwe sheria kali na kutoa funzo kwa wengine,” amesema.

Amefafanua kuwa viumbe hao hawaruhusiwi kuvuliwa isipokuwa kwa utafiti maalum unaofanywa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tafiri) au mwanafunzi anayekuwa na kibali maalum anaruhusiwa kuvua na kufanya utafiti.

Ametaja sababu ya kupotea kwa viumbe hao kuwa ni uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uvuvi haramu kwa utumiaji baruti.

“Ukipiga mabomu kuvunja miamba viumbe hao unaharibu makazi yao.

Taka za sumu toka kwenye meli na viwandani zinazoelekezwa kwenye maji.

Uchimbaji mafuta na gesi majini,” amesema.

Pia utumiaji wa nyavu haramu kwa wavuvi wadogo na wakubwa.

Habari Zifananazo

4 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button