Sheria kulinda taarifa binafsi za kimtandao yaiva

Nape Nnauye

WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, amesema mchakato wa kutungwa kwa sheria ya kulinda taarifa binafsi za kimtandao umepata kibali,  ambapo muswada huo utawasilisha  bungeni Septemba 13, mwaka huu.

Akizungumza katika kongamano la siku mbili lililowakutanisha wadau wa teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka nchi mbalimbali Afrika, Waziri nape amesema muswada huo utapelekwa bungeni kwa ajili ya kusomwa kwa mara ya kwanza, baada ya Baraza la Mawaziri kuridhia sheria hiyo itungwe.

Amesema muswada huo utakapokamilika utasaidia taarifa za watu binafsi kutotoka nje, ili kuondoa tatizo la baadhi ya watu wanaotumia vibaya mitandao na baada ya muswada huu kupelekwa bungeni, wadau watatoa maoni yao.

Advertisement

Kuhusu kongamano hilo amesema litaelimisha mambo mbalimbali ya TEHAMA, ili kubadilishana uzoefu wa wadau sekta hiyo, wakiwemo wa miundombinu kutoka ndani na nje ya nchi.